Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ali Fayyadh, mbunge na mwanachama wa Kundi la “Uaminifu kwa Muqawama”, wakati wa hafla ya kumbukumbu iliyoandaliwa na Hizbullah kwa ajili ya shahidi Saeed Ahmad Abd Nasser Abdullah katika Husseiniyya ya Al-Hadi (as) katika eneo la Ouzai, na kuhudhuriwa na idadi ya wanazuoni, shakhsia mbalimbali, wanaharakati wa kijamii, familia za mashahidi na kundi la wananchi, alisisitiza kwamba; maendeleo ya matukio yameonesha kuwa; uongozi wa Lebanon unaelekea kwenye ukingo wa mazungumzo ya moja kwa moja; njia ambayo sasa imekuwa kama mkwamo unaouhangaisha na kuusumbua, ndani ya njia hiyo bila ya kupata mafanikio yoyote unakubali makubaliano ya hatari; makubaliano ambayo yanafungua upeo wa matokeo yenye hatari kubwa kwa hali nzima ya Lebanon, iwe katika ngazi ya dola au katika ngazi ya jamii.
Alisema: Kile ambacho Waisraeli wanakitafuta ni kuwapeleka Walebanoni kwenye mlipuko wa mgogoro wa wazi baina yao wenyewe ili kuigeuza Lebanon kuwa vipande vilivyotawanyika, hali hiyo itawawezesha kutenganisha sehemu ya ardhi ya Lebanon, kuamsha mielekeo ya kujitenga, na kuunda upya hali nzima ya Lebanon kwa namna inayolingana na matakwa na eneo la ushawishi wa Israel.
Fayyadh aliongeza kuwa: Waisraeli wanajua vizuri kwamba uongozi wa Lebanon hauna uwezo wa kutekeleza ahadi ambazo unazikubali, katika kila duru ya mazungumzo, wanapata marupurupu zaidi, kisha wanayageuza marupurupu hayo kuwa wajibu na ahadi rasmi, na baadaye wanaitaka serikali ya Lebanon iyatekeleze, ni wazi kabisa kwamba mwenendo huu utaendelea mpaka hali ya Lebanon ilipuke na kuingia katika mgogoro mkubwa, haya yote yanatokea huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kupitia mauaji ya halaiki, uharibifu, kubomoa miundombinu, kusawazisha ardhi na kufanya mauaji ya kulenga watu maalumu, bila ya uongozi huu kuonesha hata kiwango kidogo cha umakini au mwitikio wowote, isipokuwa maneno matupu kuhusu usitishaji vita.
Mwanachama huyo wa Kundi la Muqawama alisisitiza kwamba; uongozi wa Lebanon unapaswa kuuchukulia kwa uzito wito wa Katibu Mkuu wa Hizbullah wa kushirikiana kwa msingi wa juhudi za pamoja kwa ajili ya kutimiza madai matano ya Lebanon. Alisema madai hayo yanapaswa kugeuzwa kuwa misingi isiyobadilika ya msimamo wa kitaifa na yafanyiwe kazi kwa lengo la kujenga msimamo wa kitaifa na wa watu wote kwa pamoja; msimamo ambao kila upande utasimama juu ya msingi mmoja wa pamoja ili ardhi irejeshwe na uthabiti na utulivu vihifadhiwe.
Maoni yako